Mafanikio ya Kimataifa kwa UAE: Wadi Wurayah, Fujairah Yaorodheshwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO
FUJAIRAH, UNITED ARAB EMIRATES, July 28, 2026 /EINPresswire.com/ -- FUJAIRAH, Umoja wa Falme za Kiarabu, 28 Julai 2026:
FUJAIRAH, Falme za Kiarabu, 28 Julai 2026: Serikali ya Falme za Kiarabu imepata mafanikio mapya ya kimataifa baada ya Wadi Wurayah katika Emirate ya Fujairah kuorodheshwa rasmi kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO, kufuatia kuidhinishwa kwa usajili wake wakati wa kikao cha 48 cha Kamati ya Urithi wa Dunia kilichofanyika mjini Busan, Jamhuri ya Korea.
Utambuzi huu wa kimataifa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaonesha umuhimu wa kimataifa wa Wadi Wurayah iliyoko Fujairah kama moja ya maeneo muhimu ya urithi wa asili duniani, na kuthibitisha nafasi yake miongoni mwa maeneo ya kipekee ya urithi wa asili wa dunia.
Mtukufu Sheikh Mohammed bin Hamad Al Sharqi, Mwanamfalme Mrithi wa Fujairah na Balozi wa jalada la uteuzi wa Wadi Wurayah kwa UNESCO, alieleza kuwa mafanikio haya ya kihistoria ni hatua muhimu katika historia ya mafanikio ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Emirate ya Fujairah. Alisisitiza kuwa huu ni wakati wa kipekee katika safari ya maendeleo na hadhi ya kimataifa ya taifa, unaoakisi dhamira thabiti ya UAE ya kuhifadhi na kulinda maeneo yake ya urithi wa asili kwa kuzingatia viwango bora vinavyotambulika kimataifa.
Mtukufu Sheikh Mohammed alisema kuwa wakati huu wa kujivunia unaakisi maono ya Serikali ya Fujairah chini ya uongozi wa Mtukufu Sheikh Hamad bin Mohammed Al Sharqi , Mjumbe wa Baraza Kuu la Shirikisho na Mtawala wa Fujairah, ya kuhifadhi eneo hili kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa binadamu pamoja na utajiri wake wa kihistoria, kitamaduni na kiasili. Alibainisha kuwa Wadi Wurayah sasa ni mfano wa kimataifa unaotambuliwa na kuthaminiwa duniani, na pia ni nyongeza muhimu inayozidi kuimarisha hadhi na sifa ya Falme za Kiarabu katika jukwaa la kimataifa.
Mtukufu Sheikh Mohammed pia alisisitiza kuwa kuorodheshwa kwa Hifadhi ya Wadi Wurayah kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO kunathibitisha umuhimu wake wa kipekee kutokana na sifa zake za kipekee za kimazingira na kijiolojia, pamoja na thamani yake kubwa ya kisayansi, kimazingira na kitamaduni. Alieleza kuwa mafanikio haya yanaakisi juhudi za Falme za Kiarabu (UAE) na Emirate ya Fujairah katika kuhifadhi maeneo yenye Thamani Bora ya Kipekee kwa Ulimwengu (Outstanding Universal Value), kuimarisha na kulinda mfumo wa ikolojia, pamoja na kuhakikisha usalama na uendelevu wake kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mtukufu Sheikh Mohammed alisisitiza pia umuhimu wa eneo hilo kama mfumo wa ikolojia uliokamilika na wenye uwiano, unaodhihirisha maelewano kati ya binadamu na mazingira yake katika kipindi chote cha historia. Alieleza kuwa Wadi Wurayah ni mfumo hai wa kipekee unaoendeleza michakato muhimu ya asili kwa muda mrefu, huku ukiendeleza maono ya kitaifa ya Falme za Kiarabu (UAE) ya kuhimiza uwajibikaji wa pamoja katika ngazi ya kitaifa na kimataifa ili kulinda urithi wa asili na kufanikisha maendeleo endelevu.
Kwa upande wake, Mhe. Sheikh Salem bin Khalid Al Qassimi, Waziri wa Utamaduni na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UAE ya Elimu, Utamaduni na Sayansi, alisema:
“Kuorodheshwa kwa Wadi Wurayah kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO ni mafanikio ya kimkakati kwa taifa ambayo yanaendelea kuimarisha nafasi ya Falme za Kiarabu kama kinara katika kulinda urithi wa asili na kuhifadhi bioanuwai. Mafanikio haya yanadhihirisha maono ya kitaifa yanayoweka urithi katika kiini cha utambulisho wa taifa, yanauona kama nguzo muhimu ya maendeleo endelevu, na yanatambua kuwa kuuhifadhi ni jukumu la pamoja kwa manufaa ya binadamu wote na vizazi vijavyo.
Kama eneo la tatu la UAE kuorodheshwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia, na la kwanza kutambuliwa kutokana na thamani yake ya kipekee ya urithi wa asili, Wadi Wurayah inaongeza uwepo wa Falme za Kiarabu kwenye ramani ya urithi wa dunia. Pia inaakisi mafanikio ya mkakati wa nchi katika kulinda rasilimali za asili huku ikitumia kikamilifu thamani yake ya kisayansi, kielimu na maendeleo.”
Mhe. Sheikh Salem bin Khalid Al Qassimi aliongeza:
“Mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za pamoja za kitaifa, ambapo Tume ya Taifa ya UAE ya Elimu, Utamaduni na Sayansi ilitekeleza jukumu muhimu katika kuratibu mchakato huo. Tume iliunganisha juhudi za Wizara ya Utamaduni, Mamlaka ya Mazingira ya Fujairah, pamoja na taasisi nyingine husika, huku ikiimarisha ushirikiano na UNESCO. Uratibu huu wa kitaasisi umeonyesha wazi Thamani Bora ya Kipekee kwa Ulimwengu (Outstanding Universal Value) ya Wadi Wurayah, na kustahili kwake kutambuliwa kama sehemu ya Urithi wa Dunia.”
Mhe. Sheikh Salem bin Khalid Al Qassimi alisisitiza kuwa Wadi Wurayah, yenye utajiri mkubwa wa bioanuwai na mifumo adimu ya ikolojia, ina umuhimu unaovuka mipaka yake ya kijiografia. Kama rejea muhimu ya kiasili na kisayansi, eneo hili linachangia kuendeleza maarifa ya binadamu. Alieleza kuwa hadhi yake kama Urithi wa Dunia wa UNESCO itapanua fursa za ushirikiano wa kimataifa, kubadilishana utaalamu na kuzalisha maarifa ya kitaalamu, huku ikiifanya dunia kutambua zaidi uzoefu wa Falme za Kiarabu (UAE) katika kulinda na kusimamia urithi wa asili kwa njia endelevu.
Mhe. Dkt. Ahmed Hamdan Al Zeyoudi, Mkurugenzi wa Ofisi ya Mtukufu Mwanamfalme Mrithi wa Fujairah, alisema kuwa mafanikio haya ya kihistoria ni hatua kubwa inayodhihirisha dhamira thabiti ya Serikali ya Fujairah katika kulinda na kuhifadhi Wadi Wurayah, pamoja na juhudi zake endelevu za kusimamia eneo hilo kwa kuzingatia viwango vya juu vya kimataifa.
Dkt. Al Zeyoudi alisisitiza kuwa juhudi zitaendelea kuifanya Hifadhi ya Wadi Wurayah kuwa kivutio cha kimataifa kinachoonesha uhusiano wa muda mrefu na wa kipekee kati ya binadamu na mazingira ya asili, huku kikihakikisha umuhimu na urithi wake vinaendelea kuhifadhiwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mhe. Asilah Abdullah Al Mualla, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mazingira ya Fujairah, alitoa shukrani zake kwa Kamati ya Urithi wa Dunia, wajumbe wa chombo cha ushauri, pamoja na Kituo cha Urithi wa Dunia cha UNESCO, kwa kutambua kimataifa Hifadhi ya Wadi Wurayah.
Mhe. Al Mualla alisisitiza kuwa kuorodheshwa kwa eneo hilo kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO kuna umuhimu mkubwa kwa dunia nzima, kwani ni moja ya vituo muhimu vya bioanuwai na mifumo ya ikolojia katika ukanda huo. Alieleza kuwa Wadi Wurayah ndiyo mojawapo ya mifumo ya ikolojia ya asili iliyobaki ikiwa katika hali yake halisi na isiyoharibiwa katika eneo kame la vilima vya chini vya Milima ya Hajar kwenye Rasi ya Arabia, na ndiyo mfano bora zaidi wa mazingira hayo ya kipekee.
Mhe. Al Mualla aliongeza:
Wadi Wurayah ni mojawapo ya maeneo machache nchini Falme za Kiarabu (UAE) yenye vyanzo vya kudumu vya maji yanayotiririka juu ya ardhi, na ndiyo makazi ya maporomoko ya maji ya asili ya kudumu pekee nchini. Hifadhi hii pia ni makazi ya idadi kubwa ya wanyama, mimea, reptilia na wadudu adimu na walio katika hatari ya kutoweka, pamoja na aina kadhaa za mamalia na ndege wanaopatikana katika eneo hili pekee.
Hali hii inaifanya Wadi Wurayah kuwa mfano bora wa michakato muhimu ya ikolojia ambayo, kwa karne nyingi, imeunda na kuendeleza mifumo ya ikolojia ya nchi kavu, maji baridi, maeneo ya pwani na baharini, pamoja na jamii mbalimbali za mimea na wanyama.”

Orient Planet Group
Orient Planet Group
email us here
Legal Disclaimer:
EIN Presswire provides this news content "as is" without warranty of any kind. We do not accept any responsibility or liability for the accuracy, content, images, videos, licenses, completeness, legality, or reliability of the information contained in this article. If you have any complaints or copyright issues related to this article, kindly contact the author above.